Happy Valley Foundation
My blogs
| Industry | Education |
|---|---|
| Location | Morogoro, Tanzania |
| Introduction | Happy Valley Foundation ni asasi binafsi iliyojikita kwenye, pamoja na mambo mengine, kuleta ufanisi wa hali ya juu katika sekta ya elimu nchini Tanzania. Happy Valley Day Care Center iliyopo Morogoro mjini inamilikiwa na kuendeshwa na Happy Valley Foundation na vipaumbele vyake ni pamoja na: Ubora wa elimu ya darasani, maadili na stadi za kujiamini na kujitegemea katika maisha binafsi ya kila siku kwa wanafunzi. Pia shule yetu imejikita kuwajengea uwezo wanafunzi katika ubunifu, upendo, ushirikiano na uhodari katika michezo. Lengo ni kuifanya shule hii mahali salama na panapoaminika na kila mzazi, mlezi ama mtaalamu yeyote yule wa elimu ya awali. Mzazi na mwanafunzi wote ni wateja wetu wakuu, tumejikita kumfundisha na kumpa uangalizi wa hali ya juu mtoto ili mzazi afanye shughuli nyingine za maendeleo bila wasiwasi wowote. Tunawaalimu na wafanyakazi wa kutosha hivyo mwanao atakuwa katika mikono salama. Aidha shule inawataalamu waliobebea katika saikolojia ya watoto na maendeleo ya mtoto ambao wataweza kumjenga mtoto na kumsaidia kujua na kutatua matatizo yaliyo katika mfumo wa maendeleo ya watoto. |

