Sammollel

My blogs

About me

Gender Male
Industry Agriculture
Occupation Senior Agricultural Officer
Location Morogoro, Morogoro, Tanzania
Introduction Uzima wa Milele International Ministries ni huduma iliyoanza kama wazo la kuwakusanya waombaji kutoka katika madhehebu mbalimbali na kufanya maombi na huduma za pamoja bila ya kujali mipaka ya udhehebu. Ilikuwa ni Disemba mwaka 2013 wakati wazo hilo lilipotolewa na wanamaombi watatu (Renatus Philbert, Stephen Shipella na Samson Mollel) ambao ilikuwa ni desturi yao kukutana kila mara jioni kuanzia saa 12 na wakati mwingine walikaa katika kulitafakari Neno la Mungu hadi usiku wa manane. Katika makubaliano hayo pia walikubaliana kuwa Samson Mollel atakuwa ni mratibu wa kikundi hicho Baada ya kupata wazo hilo, waliamua kuwashirikisha na wanamaombi wengine ambao walikuwa wakishirikiana nao katika huduma mbalimbali hususani ile huduma ya Nuru Fellowship ya KKKT - Ngudu iliyokuwa ikiongozwa na Stephen Shipella kama Mwenyekiti na huduma nyingine ilikuwa ni “Wakarisimatiki – Katholiki” waliokuwa wakifanya huduma Ngudu mjini na katika Kigango cha Kilyaboya. Wanamaombi hawa walikubaliana na wazo hilo la kuwa na huduma ya pamoja ambayo kwa wakati huo bado haikuwa na jina.