Blogger
Jd
On Blogger since: September 2009
Profile views: 1,475

My blogs

Blogs I follow

About me

IntroductionNinashukuru kwa wewe kutembelea kwenye kurasa hii ambayo ni sawa na kutimiza ndoto zangu za kufanya mawazo na fikra zangu kusomwa na watu, Mwanzo haikuwa kazi rahisi ila kutokana na Ndugu na Marafiki kuwa karibu na kunipa moyo hatimaye nimeweza kurusha kurasa hii hewani.Ninaitwa Jennifer , ni mtoto wa kwanza kutoka familia ndogo ya wasichana wawili. Ni mtu wa kawaida sana na ni rafiki wa kila mtu. Rafiki na ndugu zangu hunielezea kama mtu anayependa kuishi kwa kutumia sheria na matakwa binafsi, naamaanisha ninapenda niishi kama mimi na sio watu wanavyotaka mimi niishi, sipendi maigizo katika maisha. Ninajua kitu gani ninataka na kila siku nimejitahidi kufanya niwezavyo ili kutimiza malengo yangu. Naamini sina maadui ila nina watu wasionielewa. Ndoto zangu siku zote ni kufanya kazi au kitu chochote kinachoweza kubadilisha maisha ya mtu mwingine kwa nia njema na hii haijalishi kiwango au muda gani ninaweza kuleta mabadiliko hayo. Napenda sana kupendwa, kusafiri, kupata marafiki wapya, kufanya kazi kwa kushirikiana ,kuchat na kujadili mambo mbalimbali, kufurahi na marafiki huku tukipata vinywaji na kuangalia sinema mbalimbali .
Google apps
Main menu