IFAHAMU KALOLENI KWA UFUPI
My blogs
| Location | MOSHI, KILIMANJARO, Tanzania |
|---|---|
| Introduction | Kata ya Kaloleni inapatikana pembezoni mwa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi katika Mkoa wa Kilimanjaro. Ipo kilometa nne (4) kusini mashariki mwa mji wa Moshi. Kaskazini imepakana na Kata ya Njoro, kusini imepakana na Kata ya Mabogini na Mashariki imepakana na Msitu wa Rau na upande wa Magharibi imepakana na Kata ya Pasua. Kupitia mitaa yake miwili: KALIMANI na KALOLENI, Kata inajumuisha maeneo ya makazi ambayo yamepimwa kisheria pamoja na maeneo mengine ambayo wakazi wanaishi pasipopimwa yaani Kalimani na baadhi ya eneo la Kaloleni. Kata pia imezungukwa na dampo la taka zote za Manispaa upande wa mashariki. Ni kata yenye wakazi wapatao 5000 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2002. |
